Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe yuko nchini China kushiriki Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea  unaofanyika jijini Beijing. 
 Mkutano huu uliondaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China kwa kushirikiana na Ofisi ya Habari ya Baraza la Taifa la nchini humo, umelenga kuzikutanisha  nchi zinazoendelea kwa lengo la kubadilishana taarifa na kujadili kwa pamoja masuala ya Haki za Binadamu.
Dkt. Mnyepe  ambaye pia aliwasilisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano huo, amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zingine duniani katika kulinda na kutetea Haki za Binadamu sambamba na kuendelea kuheshimu, na kufuata Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu kutokuingilia masuala ya ndani ya nchi.
 

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea unaofanyika jijini Beijing, China.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea unaofanyika jijini Beijing, China.
  • Sehemu ya hadhira iliyojitokeza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea wakifuatilia hotuba iliyokuwa ukitolewa na Dkt. Faraji Kasidi MnyepeSehemu ya hadhira iliyojitokeza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea wakifuatilia hotuba iliyokuwa ukitolewa na Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe