Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya mazungumzo na Taasisi mbili muhimu za kifedha na kiuchumi nchini china kwa ajili ya upatokanaji wa fedha za uwekezaji mkubwa kwenye miundo mbinu na viwanda nchini Tanzania husuan kwenye Sekta ya Kilimo.

Majadiliano hayo yalifanywa kati ya Ujumbe wa TADB ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga alipokutana na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China (China Development Bank) Bwn. Chris kwenye Mkutano uliofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China wakati wa Kongamano la Pamoja la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China.

Pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano  utakaowezesha kupatikana kwa fedha kwenye uwekezaji wa miundo mbinu ya kilimo na viwanda vidogo vidogo vya uongezaji thamani kwenye mazao ya kilimo kwa wakulima nchini.

Aidha, TADB pia ilikuwa na majadiliano ya kina na Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa Vhina (China African Development Fund) ambao hufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na ya kibiashara (Equity investmenta) kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Kusoma zaidi bofya hapa.

  • Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Makamu Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China 'CADFUND". Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bwn. Francis Assenga, Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji ,Adolf Nkenda, Makamu Rais na Naibu Mtendaki Mkuu wa CadADFUND, Wang Yong na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja.

  • Kutoka kushoto ni Michael Kitulizo (Mtendaji Mkuu wa Mema Holdings), Mhe. Mbelwa Kairuki (Balozi wa Tanzania Nchini China ) Prof. F. Lekule (Mtendaji Mkuu wa International Tanfeeds Ltd), Francis Assenga (Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kilimo -TADB) wakati wa Kongamano la Biashara Viwanda na Uwekezaji kati ya China na Tanzania, mjini Guangzhou China juzi.